Skip to content
March 20, 2023
  • Facebook
  • Twitter
  • Linkedin
  • Youtube
  • Instagram
Bunda FM

Bunda FM

Ngurumo ya jamii

Connect with Us

  • Facebook
  • Twitter
  • Linkedin
  • Youtube
  • Instagram

Tags

Afya Burudani Kimataifa Kitaifa Makala Michezo Muziki Siasa Uchumi na Biashara

Categories

  • Afya
  • Burudani
  • Kimataifa
  • Kitaifa
  • Makala
  • Michezo
  • Muziki
  • Siasa
  • Uchumi na Biashara
  • Home
  • Habari Zote
  • Kitaifa
  • Kimataifa
  • Michezo
  • Siasa
  • Uchumi na Biashara
  • About us
  • Contact
STAFF LOGIN
  • Home
  • Simba Yaleta Mchezaji Mpya
  • Burudani
  • Kitaifa
  • Michezo

Simba Yaleta Mchezaji Mpya

gasper June 7, 2022 2 min read

Mabosi wao wanazidi kukuna kichwa ili kutengeneza timu itakayofukia mashimo yote yaliyojitokeza msimu huu na kushindwa kutimiza malengo yao na moja ni kusaka wachezaji wa kiwango cha juu wa kuweza kurejesha heshima hiyo.

Kama wewe ni shabiki wa Simba, basi zikufikie tu taarifa, mabosi wa klabu hiyo mezani kwao wana majina wanne ya viungo washambuliaji ambao mmoja wao atashushwa mambo yakikamilika ambaye ni Morlaye Sylla anayekipiga kwa sasa AC Horoya ya Guinea.

Sylla aliyewahi kucheza soka la kulipwa Ureno, ni moja kati ya machaguo matatu ya kwanza katika majina hayo manne na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kuna mambo mazuri yapo njiani.

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kimelidokeza Mwanaspoti, raia huyo wa Guinea anapigiwa hesabu na mabosi wa Simba kutokana na kumfuatilia kwa muda mrefu ili kumshusha Msimbazi, akiwa ni chaguo la tatu.

Kiwango anachoonyesha Sylla kwenye timu ya taifa pamoja na klabu yake ya Horoya kinatajwa ndicho kilichowavutia mabosi wa Simba na kuanza mchakato wa kumfuatilia kwa kutafuta taarifa zake mbalimbali.

“Kweli tunahitaji kiungo mwingine mshambuliji aliyekuwa kwenye kiwango bora kwa sasa na Sylla ametuvutia, ngoja tuone kama inawezekana kupatikana kwani ni mmoja wa wachezaji wazuri,” kilisema chanzo chetu makini (jina limehifadhiwa).

“Tunahitaji kiungo aina ya Sylla ili kuongeza nguvu mbele ya Clatous Chama na Rally Bwalya ambaye huenda tusiwe naye msimu ujao kutokana na dili lake la kuuzwa Amazulu limefikia mahala pazuri.”

Sylla amekuwa kwenye kiwango bora kwenye Ligi Kuu ya Guinea ikionyesha ubunifu wa kupiga pasi za mwisho, kuanzisha mashambulizi, mzuri anapokuwa na mpira mguuni, mbunifu pamoja na kuwasumbua viungo wa timu pinzani.

Kiungo huyo alianza soka la vijana katika klabu ya E. Tanene kisha kutua Arouca ya Ureno kabla ya kurudia CO de Coyah ya kwao Guinea mwaka 2019 kabla ya kutua AC Horoya aliyonayo hadi sasa.

Akiwa na umri wa miaka 23 tu, tayari mwamba huyo ameshachukua tuzo mbalimbali ikiwemo za mchezaji bora wa mechi, huku akizichezea timu za taifa ya Guinea akianza na timu ya vijana U17 mwaka 2015 na kucheza mechi tatu na kufunga nao moja.

Pia amewahi kukipiga U20 2017 akicheza mechi nane na kufunga mabao mawili na sasa yupo timu ya wakubwa akiichezea michezo nane na kufunga mabao matatu.

Simba inahitaji kiungo wa ushambuliaji raia wa kigeni kutokana na kutofurahishwa na wachezaji wanaocheza kwa sasa katika eneo hilo msimu huu wakiwemo, Chama, Bwalya na wengineo.

Machaguo mawili ya kwanza kwa mabosi wa Simba walipanga kumsajili, Victorien Adebayor wa USGN na Stephane Aziz Ki na imekuwa ngumu kwao kutokana na nyota hao kuhitajika na timu nyingine ikiwamo Yanga na RS Berkane.

Adebayor anaweza akatua RS Berkane ya Morocco iliyomwekea mkwanja mrefu zaidi ya ule ambao Simba inaweza kutoa, wakati Ki wa Asec Mimosas inaelezwa huenda akatua Yanga.

gasper

See author's posts

Continue Reading

Previous: MASHARTI MAPYA KWA MKONGO
Next: Tume Ya Utawala Bora Yaing’ang’ania Polisi

Habari nyingine

1 min read
  • Kimataifa
  • Kitaifa

March 12, 2023
RAPA A.K.A WA AFRIKA KUSINI AMEUAWA KWA RISASI
1 min read
  • Burudani
  • Kimataifa

RAPA A.K.A WA AFRIKA KUSINI AMEUAWA KWA RISASI

February 11, 2023
NECTA Yasitisha Kutangaza Shule Bora na Mwanafunzi Bora
1 min read
  • Kitaifa

NECTA Yasitisha Kutangaza Shule Bora na Mwanafunzi Bora

January 29, 2023

RATIBA YA VIPINDI VYETU

  • 05:00 - 06:00 :- Hamka na Bunda FM
  • 06:00-06:30:- Habari za Ulimwengu (DW)
  • 06:30-07:00:- Ukurasa Mpya
  • 07:00-07:10:- Taarifa ya Habari
  • 07:10-10:00:- Ukurasa Mpya
  • 10:00-13:00:- Mchaka Mchaka
  • 13:00-14:00:- Habari za Ulimwengu (DW)
  • 14:00-16:00:- Ladha Kamili
  • 16:00-18:00:- Busati la Habari
  • 18:00-18:30:- Habari za Ulimwengu (DW)
  • 18:30-19:00:- Dance Africa
  • 19:00-19:10:- Taarifa ya Habari
  • 19:10-21:00:- Dance Africa
  • 21:00-22:00:- B-Sport
  • 22:00-01:00:- Planet Love
  • 01:00-04:00:- Usiku Mnene

  • Afya (2)
  • Burudani (5)
  • Kimataifa (6)
  • Kitaifa (16)
  • Makala (4)
  • Michezo (4)
  • Muziki (1)
  • Siasa (3)
  • Uchumi na Biashara (1)

Wasiliana nasi

Bunda FM LTD, 92.1 MHz
P.O. BOX 452
BUNDA-MARA
E-mail: Ngurumoyajamii@bundafm.co.tz
PNONE NO: +255 754 279 340
+255 755 029 400
+255 717 457 216

Masafa yetu

Our major frequency is 92.1 FM, whereby we cover regions of Mara, Simiyu, Mwanza, Geita,Kagera, Shinyanga, Singida, Tabora and Katavi regions.

  • Home
  • Habari Zote
  • Kitaifa
  • Kimataifa
  • Michezo
  • Siasa
  • Uchumi na Biashara
  • About us
  • Contact
Copyright © All rights reserved. | DarkNews by AF themes.