Skip to content
March 20, 2023
  • Facebook
  • Twitter
  • Linkedin
  • Youtube
  • Instagram
Bunda FM

Bunda FM

Ngurumo ya jamii

Connect with Us

  • Facebook
  • Twitter
  • Linkedin
  • Youtube
  • Instagram

Tags

Afya Burudani Kimataifa Kitaifa Makala Michezo Muziki Siasa Uchumi na Biashara

Categories

  • Afya
  • Burudani
  • Kimataifa
  • Kitaifa
  • Makala
  • Michezo
  • Muziki
  • Siasa
  • Uchumi na Biashara
  • Home
  • Habari Zote
  • Kitaifa
  • Kimataifa
  • Michezo
  • Siasa
  • Uchumi na Biashara
  • About us
  • Contact
STAFF LOGIN
  • Home
  • Sababu risiti za EFD kufutika maandishi yatajwa
  • Kitaifa

Sababu risiti za EFD kufutika maandishi yatajwa

Bundafm June 20, 2022 1 min read

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Hamad Hassan Chande imetaja sababu za kufutika kwa maandishi  kwenye risiti za mashine ya kodi ya kielektroniki (EFD) kwamba inatokana na kuchapwa kwenye karatasi zisizokuwa na ubora.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatatu Juni 20, 2022 akibainisha kuwa serikali inalifanyia kazi suala hilo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu,  Angelina Malembeka aliyetaka kujua  mpango wa serikali kuboresha risiti za mashine hizo ili zisifutike baada ya muda mfupi.

“Kufutika huko baada ya muda mfupi kumesababishwa na matumizi ya karatasi zenye ubora hafifu,”amesema Chande.

Amesema baada ya kubaini changamoto hiyo, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato (TRA) imeshatengeneza viwango vya ubora wa karatasi hizo vinavyotakiwa.

Ameeleza kuwa kwa sasa wanaendelea na usimamizi kuhakikisha karatasi zote zinakidhi ubora unaotakiwa.

Kingine ametaja kuwa TRA imeboresha mfumo wa usimamizi wa mashine za EFD kwa kuuwezesha kupokea taarifa zote za kila risiti inayotolewa na kuitunza katika kifaa cha kutunza kumbukumbu na hivyo kuwezesha nakala ya risiti hizo kuweza kupatikana wakati wowote inapohitajika.

Bundafm

See author's posts

Continue Reading

Previous: Mapacha Wenye Miaka 9 Mkoani Arusha Wanaishi Kwa Kula Magodoro
Next: Kesi ya Sabaya yaahirishwa tena

Habari nyingine

1 min read
  • Kimataifa
  • Kitaifa

March 12, 2023
NECTA Yasitisha Kutangaza Shule Bora na Mwanafunzi Bora
1 min read
  • Kitaifa

NECTA Yasitisha Kutangaza Shule Bora na Mwanafunzi Bora

January 29, 2023
Matokeo kidato cha nne 2022 yatangazwa, haya hapa
1 min read
  • Kitaifa

Matokeo kidato cha nne 2022 yatangazwa, haya hapa

January 29, 2023

RATIBA YA VIPINDI VYETU

  • 05:00 - 06:00 :- Hamka na Bunda FM
  • 06:00-06:30:- Habari za Ulimwengu (DW)
  • 06:30-07:00:- Ukurasa Mpya
  • 07:00-07:10:- Taarifa ya Habari
  • 07:10-10:00:- Ukurasa Mpya
  • 10:00-13:00:- Mchaka Mchaka
  • 13:00-14:00:- Habari za Ulimwengu (DW)
  • 14:00-16:00:- Ladha Kamili
  • 16:00-18:00:- Busati la Habari
  • 18:00-18:30:- Habari za Ulimwengu (DW)
  • 18:30-19:00:- Dance Africa
  • 19:00-19:10:- Taarifa ya Habari
  • 19:10-21:00:- Dance Africa
  • 21:00-22:00:- B-Sport
  • 22:00-01:00:- Planet Love
  • 01:00-04:00:- Usiku Mnene

  • Afya (2)
  • Burudani (5)
  • Kimataifa (6)
  • Kitaifa (16)
  • Makala (4)
  • Michezo (4)
  • Muziki (1)
  • Siasa (3)
  • Uchumi na Biashara (1)

Wasiliana nasi

Bunda FM LTD, 92.1 MHz
P.O. BOX 452
BUNDA-MARA
E-mail: Ngurumoyajamii@bundafm.co.tz
PNONE NO: +255 754 279 340
+255 755 029 400
+255 717 457 216

Masafa yetu

Our major frequency is 92.1 FM, whereby we cover regions of Mara, Simiyu, Mwanza, Geita,Kagera, Shinyanga, Singida, Tabora and Katavi regions.

  • Home
  • Habari Zote
  • Kitaifa
  • Kimataifa
  • Michezo
  • Siasa
  • Uchumi na Biashara
  • About us
  • Contact
Copyright © All rights reserved. | DarkNews by AF themes.