
Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, imesema malalamiko ya rushwa wakati mwingine hutokana na wananchi kutojua sheria na taratibu.

Akizungumza katika Mahojiano Maalum na Bunda FM , Naibu Msajili wa Mahakama hiyo,Frank Leonard Moshi amesema kutokujua taratibu kuwafanya wananchi kudhani wanazungushwa kwa nia ya kutakiwa watoe rushwa.
Wakati huo huo, Mkaguzi wa Polisi, Adam Khalfan, amesema Jeshi hilo limekuwa likiwashirikisha wananchi wa kawaida kutokomeza uhalifu wilayani Bunda kupitia Polisi Jamii.

Hata vivyo, Polisi na mahakama wamewataka wananchi kutumia Maadhimisho ya Wiki ya Sheria,kujielimisha; Kaulimbiu ya wiki ya sheria mwaka huu ni ‘Umuhimu wa utatuzi wa migogoro na kukuza UCHUMI’.