Na Jenipher Hassan
Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Nassari ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzaia (TRA) wilaya ya Bunda kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha mwaka 2022.
Nassari ametoa pongezi hizo wakati akisoma taarifa ya utekelezwaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2021 na Januari hadi Disemba 2022 mbele ya Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Bunda Mayaya Abraham.
Katika kipindi Julai hadi Disemba mwaka 2021 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Bunda imekusanya Tsh Bil 2.07 sawa na 110% huku ikikusanya jumla ya Tsh Bil. 4.48 kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 ambazo ni sawa na 111.8%