MARA INRENATIONAL BUSINESS EXPO
Uchumi wa Mkoa wa Mara kupaa baada ya Maonesho ya Septemba
Na Conges Mramba,Bunda FM Radio
Kamati ya Mandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara mkoani Mara imesema Mkoa huu utarejea katika hadhi yake ya kiuchumi ya miaka ya 80 mkoa ulipokuwa na viwanda vikubwa vya nguo, vya Maziwa,Mahoteli makubwa ya kitalii na vinu vya kuchambulia pamba.
Wakizungumza juzi na waandishi wa Habari, serikali na wadau wa Biashara wamesema, wanakusudia kupitia Maonesho Makubwa ya Biashara ya Kimataifa hapa mjini Musoma, mapema mwezi Septemba, viwanda vikubwa mithili ya Musoma Textiles(Mutex) na vingine vilivyokuwa vikichakata Maziwa, maarufu sana hapa nchini na nchi jirani kama “ Maziwa ya Mara”,vinu vya kuchambulia pamba na mazao mengine ya kimkakati,vitafufuliwa.
Aidha, Aidha, wadau hawa wanasema zamani kulikuwa na Mahoteli makubwa ya kitalii hapa mjini Musoma kama Hoteli iliyokuwa ikimilikiwa na Shirika la Reli(TRC) zama zile ,lakini sasa vyote havipo,na wanamatumaini baada ya maonesho haya mahoteli kama haya yatafufuliwa ili kuongeza ajira na kipato kwa wakazi wa mkoa huu.
Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Uzalishaji,Dk. Noel Crispine Komba, anasema viwanda vikubwa kama Mutex na vya maziwa na vile vya kuchambulia pamba vimekufa na kudumaza uchumi kwa wakazi wa mkoa huu takriban milioni mbili,.
Mkoa huu sasa unakisiwa kuwa na na Pato la jumla (GDP)ambalo ni takriban shilingi Bilioni tano kwa mwaka.
Dk.Komba amesema katika Mkutano na waandishi wa Habari,Julai 19 mwaka huu kwamba, matumaini ya mkoa huu ni kutumia Maonesho ya Kimataifa ya Bishara, MARA INTERNATIONAL BUSINESS EXPO, kufufua viwanda vya zamani vya Ngozi,vya maziwa,vya kusindika pamba na mafuta ya kula, na vingine vua kusindika samaki wengi na watamu wanaopatikana ziwa Victoria ili kusisimua uchumi wa Mkoa.
“Tunakusudia viwanda na taasisi zilizokufa ama kudumaa zitapata wawekezaji na Biashara nyingine zitapata wabia wa biashara na kunyanyuka kupitia maonesho haya yanayokusudia kuleta makampuni 200 ya ndani na nje ya nchi,bila kusahau Balozi za Afrika Mashariki,Zimbabwe,Marekani na nchi za Mashariki ya Mbali”,Dk. Komba amefafanua.
Hata hivyo,Mwenyekiti wa Chama cha Wafanya Biashara,Wenye Viwanda na Kilimo)TCCIA,Mkoa wa Mara, Boniface Ndengo alisema Halmashauri nne za Mkoa wa Mara kati ya sita,huzungukwa na ziwa kubwa kuliko maziwa yote Barani Afrika,na ziwa la Pili Duniani kuwa na maji yasiyo na chumvi,nyuma ya ziwa la Superior lililoko Marekani,Ziwa Victoria.
Ndengo anasema, Mkoa wa Mara unatakiwa kutumia Uchumi wa Bluu kuinua uchumi wa watu “Hata Rais Samia Suluhu Hassan alipozungumza juzi alisisitiza kuhusu ‘Uchumi wa Bluu’ sasa sisi Mara tunazungukwa na ziwa hili kubwa na maarufu duniani ambalo ni nyumba ya samaki wengi watamu,na ni chanzo cha Mto maarufu Duniani,Mto Nile unaotiririka kuanzia hapa hadi hadi Bahari ya Kati”,Ndengo amefafanua.
Aidha,Mkuu huyu wa TCCIA anasema,licha ya kuwepo migodi ya madini ya dhahabu, Hifadhi na mapori tengefu,fukwe za ziwa hili,kilimo cha pamba,uvuvi,ufugaji,na kuwajirani na nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC)na jumuiya ya SADC kuuza mazao anuwai yanayopatikana hapa katika masoko hayo makubwa.
“Mkoa wa Mara unapakana na Hifadhi ya Serengeti ambayo imepata tuzo ya Ubora miaka mitatu mfululizo,na asilimia 70 ya Hifadhi hii iko hapa kwetu,tunafukwe nzuri,tuna madini,kilimo cha pamba,tuna makabila zaidi ya 20 katika mkoa mmoja na kuna vivutio vingi vya kitamaduni na kitalii(Cultural Tourism),ambavyo vinaweza kufanya matajiri wakubwa wa Ukanda huu wa Afrika watoke Mara,maana kuna kila fursa na rasilimali”,amesema Ndengo.
Aidha, Mratibu Mkuu wa Maonesho haya, Bernard Mwata, amesema zaidi ya makampuni ya biashara kubwa,za kati na Ndogo (SMEs) yaliyoalikwa katika Maonesho haya ya Kimataifa ya Mara International Business Expo, yatazalisha ajira mpya kwa vijana wanaohitimu masomo katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
Hata hivyo,Mwata amesema wakati wa maonesho haya kutakuwa na Mashindano ya Mbio Ndefu za Riadha, Marathon kwa wanawake kwa lengo la kutangaza Hifadhi ya Serengeti.
Aidha, Mbunge wa Musoma mjini,Vedastus Manyinyi Mathayo,amesisitiza kwamba wakazi wa Mkoa wa Mara watumie Maonesho haya kukutana na wafanyabiashara wageni kuingia ubia wa kibiashara na kujifunza namna ya kutanuka kibishara ndani na nje.
The Mara International Business Expo yataanza mapema Septemba Pili ha 11 katika viwanja vya Michezo vya Karume mjini Musoma na kumalizika Septemba 11.
Wageni takriban 100,000 wa ndani na nje ya nchi zikiwemo Balozi za mataifa ya Afrika na Mashariki ya Mbali,yamealikwa kuhudhuria maonesho haya.
Maonesho haya ambayo yana Kauli Mbiu, “BRINGING TOGETHER INVESTORS FOR FUTURE GROWTH”, yaani kuwaleta pamoja wawekezaji kwa ajili ya Maendeleo ya siku za Usoni hapa mkoani Mara,
Sekta anuwai za biashara,Kilimo,Madini,Uvuvi,Utalii na Ujasiliamali zimealikwa kushiriki maonesho haya yanayokususdia kuwakutanisha watanzania na makapuni makubwa kadiri 500 hapa mkoani Mara.
TCCIA wa nasema Mkoa Wa Mara unatajwa kuwa mithili ya ‘Silicon Valley’ huko Marekani mahali kuliko na dhahabu,samaki,wanyamapori wa kupendeza mashamba ya kilimo ambacho ni mali ghafi za viwanda vya bidhaa nyingi,ambapo matajiri wakubwa duniani wanaweza kutokea hapa kwenye wingi wa rasilimali.
Hata hivyo,wachambuzi wa masuala ya uchumi wamesema Mara ni mkoa ambao sasa ni Dubwana lililolala(SLEEPING GIANT)lakini linaweza kunyanyuka kupitia maonesho haya ambayo yanatazamiwa kusisimua fursa zake nyingi kama mifugo,uvuvi,kilimo cha pamba,madini,ziwa la Kihistoria,mito mikubw akama Mara unaoanzia Misitu ya Maao huko Kenya na kumwaga maji yake ziwani Victoria kilomita chache tu Kaskazini mwa mji wa Musoma,Hifadhi ya Serengeti,Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyoko Butiama,n.k