Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022, Tanzania Bara na Visiwani.
Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema watahiniwa wa Shule 456,975 kati ya Watahiniwa 520,558 wenye matokeo ambao ni sawa na 87.79% wamefaulu kwa kupata madaraja kuanzia daraja la kwanza, hadi la nne
“Kati yao Wasichana 243,285 (87.08%) na Wavulana ni 213,690 (88.60%), ufaulu huu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa 0.49% ikilinganishwa na mwaka 2021”
Aidha Baraza la Mitihani (NECTA) limefuta matokeo yote ya Watahiniwa wanne wa kidato cha nne mwaka 2022 walioandika lugha za matusi katika mitihani yao.
Baraza la Mitihani pia limeyafuta matokeo yote ya Watahiniwa 333, mmoja wa QT na 332 wa Mtihani wa kidato cha nne ambao wamebainika kuwa wamefanya udanganyifu kwenye mtihani
“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 (2) (I na J) cha Sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 (2) (b) cha kanuni za mtihani mwaka 2016”