
Na Jenipher Hassan
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya Bunda LEONARD ELIAS MAGWAYEGA, Amesikitishwa na ujenzi wa choo na jengo la kufulia nguo katika kituo cha Afya Mugeta Kata ya Mugeta Wilayani Bunda kushindwa kukamilika kwa wakati.

Akiwa katika ziara ya maadhimisho ya miaka 46 ya chama cha Mapinduzi CCM, ngazi ya wilaya katika ofisi ya kata ya Mugeta, amesema mwaka 2020 serikali ilitoa fedha million 22 kwaajili ya ujenzi.
Aidha amesema tarehe 19/01/2023 mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM, Mhe. MAYAYA ABRAHAM MAGESSE, alitoa agizo kwa viongozi wa kata hiyo kufikia tarehe 31/01/2023 ujenzi wa choo uwe umekamilika.
Pia viongozi wa CCM wilaya wameshiriki zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Halmashauri ya wilaya Bunda na katika kituo cha Afya Mugeta, na zaidi ya miti 500 imepandwa.