MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KAMALA HARRIS ANAKUJA TANZANIA 🇹🇿 🇺🇸
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kuzuru Tanzania mwezi huu ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika katika nchi za Ghana, Tanzania na Zambia inayotarajiwa kufanyika Machi 25 hadi Aprili 3. Ziara hiyo inaakisi kuibuka tena kwa Tanzania kama nguvu kuu ya kijiografia tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipochukua madaraka miaka miwili iliyopita Mnamo Aprili 2022,. Samia na Kamala walikutana Ikulu ya Washington DC