Rapa Kiernan Forbes anayefahamika kwa jina la AKA ameuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Florida, Durban Afrika Kusini
Polisi wamethibitisha kuuawa kwa mwanamuziki huyo wa Afrika Kusini, mwenye umri wa miaka 35, kwa kupigwa risasi 5 nje ya ukumbi wa burudani ya usiku.
Wateja wa mkahawa wa jirani na lilipotokea tukio hilo walisema AKA alikuwa amesimama nje ya Wish alipopigwa risasi.
Garrith Jamieson, msemaji wa ALS Paramedics amesema Florida Road imefungwa baada ya tukio la risasi na watu wawili wamethibitishwa kufariki.
Rapa huyo ambaye amewahi amewahi kushirikiana na wasanii wa Tanzania @diamondplatnumz MAKE ME SING lakini na @johmakinitz ngoma inayoitwa DON’T BOTHER.