Mamlaka ya Ubelgiji imekabidhi jino la kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba, kwa familia yake katika hafla iliyofanyika Brussels.
Jino hilo ni sehemu pekee ya mabaki ya mwili wake ambayo inadhaniwa kuwa bado ipo baada ya kunyongwa na kisha mwili wake kuyeyushwa kwa tindikali mwaka 1961.
Mwanasheria Mkuu, Frederic Van Leeuw aliwakabidhi familia ya Lumumba kisanduku kidogo cha rangi ya bluu kilichokuwa na jino hilo kwenye hafla hiyo iliyoonyeshwa kupitia luninga katika jumba la Egmont, Brussels.