Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Jumatatu ya September 30 2019 mtangazaji wa BBC Salim Kikeke alitangazwa rasmi kuwa balozi wa Simba SC katika jiji la London England, taarifa hizo zilitolewa kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa Simba SC na kueleza kuwa bodi ya Simba SC imeridhia na kubariki Salim Kikeke kuwa balozi wao wa kwanza.
Sasa tunajua Kikeke anaishi na kufanya kazi jijini London lakini wengi walikuwa wakijiuliza Salim Kikeke baada ya kutangazwa kuwa balozi majukumu yake ni yapi Simba SC, ubalozi wake ukoje kwa mkataba analipwa au ni kutokana na mapenzi yake kwa Simba SC, AyoTV imempata Kikeke katika exclusive interview.

“Ni heshima kubwa kama hii kuweza kuteuliwa kuwa balozi wa moja kati ya vilabu vikubwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla Simba SC, kikubwa tunachotazama lengo letu kubwa hasa ni kukuza soka la Tanzania na Afrika Mashariki, nafasi hii ni jambo jipya ni jambo geni kuwa balozi wa kwanza kabisa katika club hii majukumu yake ya kimsingi kwa sasa ni kukusanya mashabiki wa Simba SC waliopo hapa London”>>>Salim Kikeke

Author: bundafm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *