MENONITE WACHAGUANA

Mkutano Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania(KMT)uliomalizika mwezi uliopita,Umemchagua Askofu wa Dayosisi ya Mashariki,Nelson Kisare, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo.

Kulingana na Habari kutoka ndani ya Kanisa hilo,Askofu Kisare amechaguliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mwaka 2021 uchaguzi mwingine utakapofanyika tena.

Aidha, Mkutano huo uliomalizika Kitaji Mjini Musoma, umemchagua Kennedy Sigira kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Maaskofu wa KMT na Emmanuel Hagai amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu.

Naibu Katibu Mkuu aliyechaguliwa ni Musa Marwa,na Mtunza Hazina wa Kanisa hilo sasa ni Phanuel Mesha.

Wajumbe sita wa Kamati Kuu ya Kanisa hili ni Thomas Njagwa,Daudi Marara,Chirangi Mutaragara,Leah Makonyi,Mchungaji Aketch na Mary Mhochi.

Kulingana na Katiba ya Kanisa hili,viongozi waliochaguliwa kushika nyadhifa hizi watakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu hadi 2021.

Author: bundafm