Marekani yapiga marufuku wasafiri kutoka Brazil

Marekani imewapiga marufuku kuingia nchini humo, wasafiri waliokuwa nchini Brazil katika muda wa wiki mbili zilizopita. Hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi za kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona.

 Tayari utawala wa rais Donald Trump umekwizuia safari za ndege kutoka Umoja wa Ulaya, Uingereza na China. Marekani inaongoza kwa idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona, ikifuatiwa na Brazil na Urusi.

 Marufuku hiyo dhidi ya wasafiri kutoka Brazil ambayo inaanza kutekelezwa Alhamisi ijayo haiwahusu raia wa Marekani na wale wenye vibali vya kudumu vya kuishi nchini humo.

 Kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha John Hopkins, Brazil inavyo visa 347,000 vya maambukizi ya corona, ambapo watu 22,000 miongoni mwa waliopata virusi hivyo wamekwishapoteza maisha.

(via DW Swahili)

Rais Donald Trump

Author: bundafm