MADRID(Hispania)

Maelfu ya watu nchini Hispania wameshangaa kuona maelfu ya mifugo ikifanya maandamano ya hiari barabarani, na kukwamisha shughuli za usafiri katika miji mikuu kama huu Madrid.

Shirika la Habari la Uingereza, Reuters limesema,tukio la kondoo na mbuzi kujaza barabara Jumapili iliyopita,linafuatia wafugaji kuacha wanyama hao kukumbuka mapito ya kale ya wanyama hawa katika maeneo haya kabla ya kuwa miji mikuu.

 Hili ni tukio la kila mwaka lililoanza mwaka 1994, wafugaji walipokuwa wakiruhusu kondoo na mbuzi kwenda kusaka malisho Kaskazini MWA Hispania nyakati za majira ya baridi.

Njia hizi zilikuwa zikifikisha mifugo hawa hadi pande nyingine za mataifa jirani karne chache zilizopita,lakini leo njia hizo zinapita katikati ya Madrid mji mkuu wa Hispania,hususan katika mitaa maarufu.

Wafugaji wanalipishwa kiasi Fulani cha pesa  na mamlaka za mji   kama mifano ya makubaliano ya mwaka 1418;ambazo ni pesa 50 ziitwazo maravedis kwa kondoo 1,000 ili wapiti mitaa maarufu ya jiji.

Hawa mifugo ni pamoja na kondoo 2,000 aina ya Merino na mbuzi 100.

Ni hapo sasa magari na watu wanapaswa kuwapisha kondoo na mbuzi ili wafanye maandamano katika mji huu mkuu,bila shaka watu wanaweza kuchelewa makazini wanapokuwa wakisubiri maandamano ya mbuzi na kondoo kupita katika mitaa ya mji mkuu wa Madridi, Hispania.

Author: bundafm