Hispania yakaribisha watalii kutoka pande zote duniani

Hispania siyo tu inakaribisha bali inahimiza pia utalii wa kimataifa kuanzia mwezi Julai, Hayo yamezungumzwa na waziri mkuu wa nchi hiyo.

“Hispania inatarajia watalii, kuanzia mwezi Julai” Pedro Sanchez amezungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kuendelea kwa kusema kuwa “Watalii wa kigeni sasa wanaweza kuanza kupanga likizo zao kwenda Uhispania.”
Uhispania inapata wageni milioni 80 kwa mwaka, na sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 12 ya Pato la Taifa la nchi hiyo.

Mlipuko wa corona umeivuruga sekta hiyo kwani wafanyakazi milioni moja katika sekta ya utalii wamesimamishwa kwa muda.

“Uhispania inahitaji utalii na utalii unahitaji usalama. Tutahakikisha kwamba watalii hawatakuwa hatarini na hawataleta hatari yoyote kwa nchi yetu, “alisema Sanchez.

Wizara za Uchukuzi na Viwanda zinatarajiwa kutolewa mpango wa kila wiki hii kuhusu itifaki ya afya ambayo itabidi sekta ya utalii ifuate kwani virusi bado vipo.

“Ninakaribisha taasisi zote za utalii zianze kujiandaa kuanzia leo kuanza tena shughuli,” alisema Sanchez.

(via DW Swahili)

Author: bundafm