Bunda wailalamikia TCB kusambaza viuatilifu duni

Jessica Mwita na Sylvia Ndamugoba wa Bunda FM

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wameilalamikia Bodi ya  pamba  Nchini (TCB) kusambaza viwatilifu  visivyo ba ubora kwa wakulima.

Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani juzi, wamesema viuatilifu vilisvyosambazwa kwa wakulima katika msimu huu wa kilimo cha pamba vimesabisha hasara kubwa  katika msimu wa zao hilo katika msimu huu wa 2019 -2020.

Wakizungumza kwenye Baraza la madiwani, kwenye ukumbi wa halmashauri ya Mji wamesema, kutokana na viwatilifu hivyo kushindwa kuua wadudu wasumbufu, vimesababisha mavuno ya zao la pamba kushuka na kuleta hasara kubwa kwa wakulima.

Hata hivyo,Adelina Mfikwa, Ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri hii, akijibu malalamiko hayo amesema, kutokana na changamoto hizo Bodi ya Pamba haikuhusika na utoaji wa viwatilifu kwa wakulima, bali vibali hutolewa na  kuratibiwa na Taasisi nyingine kama TPRI.

Madiwani hao wameiomba serekali kusambaza  viwatilifu vyenye ubora ili kuinua kilimo cha  zao la pamba ili mkulima aweze kunufaika na zao hilo la biashara.

Bunda,ni miongoni mwa wilaya takriban 40 zinazolima zao la Pamba hapa nchini.

Author: bundafm